Entertainment

Guardian Angel Awatolea Uvivu Wanaopinga Utajiri Wake

Guardian Angel Awatolea Uvivu Wanaopinga Utajiri Wake

Mwanamuziki wa injili nchini Kenya, Guardian Angel, amewajibu vikali wakosoaji wanaopinga au kutilia shaka hali yake kiuchumi, baada ya kufichua kwamba hutumia takribani KSh 1.5 milioni kila mwezi.

Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram, Ameeleza kuwa anaishi katika mtaa wa kifahari wa Karen na pia anamiliki shamba lenye ukubwa wa ekari tano katika eneo la Lukenya.

Kwa mujibu wa Guardian Angel, Wakristo wengi hawana imani ya kuona wenzao wakifanikiwa, jambo linaloonyesha changamoto katika kuelewa baraka na mafanikio yanayotoka kwa Mungu. Anasema ataendelea kushirikisha mashabiki wake kuhusu safari yake ya maisha bila kujali maoni ya wakosoaji.

Kauli yake imeibua mjadala mitandaoni, huku baadhi wakimuunga mkono na wengine wakimshuku wakihoji kwamba msanii huyo anajinasibu na mali ya mke wake ambaye ana anagharamia Maisha yake ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *