
Hafla ya Tuzo za Grammy huenda ikafanyika April 3 au 10 mwaka huu kufuatia kuahirishwa kufanyika Januari 31 kutokana na tishio la kirusi cha Omicron.
Mtandao wa Hits Daily Double umearifu kwamba siku ya April 3 inapewa nafasi kubwa zaidi kutokana na kutokuwa na matukio mengi ya kiburudani.
Huu unakuwa mwaka wa pili mfululizo kwa tuzo hizo kuahirishwa, mwaka jana ziliahirishwa kutoka Januari na kufanyika Machi 14, mwaka wa 2021.