Gossip

Harmonize Awapa Somo Wanaume Wanaowachukulia Poa Wanawake Wao

Harmonize Awapa Somo Wanaume Wanaowachukulia Poa Wanawake Wao

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, ameamua kuwapa ujumbe mzito wanaume wanaochukulia poa wanawake waliopo kwenye maisha yao.

Kupitia ujumbe alioutoa kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amesisitiza umuhimu wa kuwajali, kuwathamini na kuwatunza wanawake wanaoonyesha mapenzi ya dhati.

Hitmaker huyo wa Leo amesema kuwa si rahisi kumpata mwanamke wa kweli mara mbili, hivyo mwanaume akimpata mwanamke mwema, anatakiwa kumheshimu, kumlinda na kumjali bila dharau au kumuumiza kihisia

Kwa mujibu wa Harmonize, wanawake wa aina hiyo ni wachache na wanapaswa kupewa heshima wanayostahili.

Mashabiki na wadau mbalimbali wameonekana kuunga mkono kauli yake, wakisema ni somo muhimu kwa wanaume wengi wanaodharau mapenzi ya kweli hadi wanapokuja kujutia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *