
Staa wa muziki wa BongoFleva Harmonize amewakata mashabiki zake kuto hangaika kupiga kura kwenye tuzo zozote.
Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize amesema kwamba hajateuliwa kwenye tuzo zozote hivyo mashabiki zake wasipoteze bando kupiga kura.
Hitmaker huyo wa “Teacher” amesema kuwa hataki kuwa miongoni mwa wasanii wanaotajwa kuwania tuzo ambazo ametajwa kuwania mwaka huu kwani waandaji wa tuzo hizo tayari wanawafahamu washindi.
Ikumbuke Harmonize kwa mwaka huu wa 2021 ametajwa kuwania tuzo za All Africa Music Awards na African Entertainment Awards USA kupitia kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki akichuana na wakali kama Diamond Platnumz, Alikiba, Otile Brown, Khaligraph Jones, Meddy, Eddy Kenzo, na The Ben.