Msanii nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, ameonesha furaha kubwa kufuatia mafanikio makubwa ya wimbo wake mpya “Leo” unaoongoza chati za majukwaa ya kidijitali nchini Tanzania na Kenya.
Kupitia mitandao ya kijamii, Harmonize amesema mafanikio hayo yametokana na kazi kubwa aliyowekeza pamoja na sapoti ya dhati kutoka kwa mashabiki wake. Amebainisha kuwa si jambo rahisi kutengeneza nyimbo zinazopendwa kila mwaka, akisisitiza kuwa anathamini sana upendo anaopokea kutoka kwa mashabiki wake.
Kutokana na mafanikio hayo, Harmonize amewahakikishia mashabiki kuwa anakuja na albamu kubwa yenye hits kali, itakayokwenda kwa jina la 31 The Album. Kwa mujibu wa wa bosi wa Konde Gang, albamu hiyo inatarajiwa kutoka kabla ya siku yake ya kuzaliwa.
Wimbo wa Leo ambao Harmonize amemshirikisha Mbosso, unaongozwa kwenye majukwaa mbali mbali ya kidijitali kama Youtube, Shazam, Apple Music, Boomplay na Spotify nchini Kenya na Tanzania.