
Mwanamuziki kutoka Congo Innos B ametangaza kuachia album yake mpya aliyoipa jina la Mortel-06 The Album.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkali huyo aliyefanya poa nchini kupitia wimbo wa Yope Remix’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz ,tayari ameshare cover photo ya album hiyo ambayo itatoka kabla ya mwaka huu kuisha.
Licha ya kuweka wazi jina na cover la album yake, Innos B hajatuambia idadi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye Mortel-06 album ambapo amesema album hiyo itaingia sokoni ” Desemba 26 mwaka huu.