
Director na mtayarishaji wa video za muziki nchini J Blessing amenyosha maelezo kuhusu kuwasaini wasanii wa kike kwenye lebo ya Digit One Music.
Katika mahojiano yake hivi karibuni J Blessing amesema wasanii wa kike wana ushirikiano mzuri kwenye suala ufanyaji kazi tofauti na wenzao wa kiume ambao kwa mujibu wake ni wabishi kupitiliza.
Sanjari na hilo amekanusha kuwa kwenye ugomvi na Bahati pamoja na Willy Paul kwa madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa wanawasiliana kila mara kweny shughuli zao kimuziki.
Utakumbuka kwa sasa Lebo ya Digit One Music imeingia ubia wa kufanya kazi na wasanii watatu wa kike ambao ni Avril, Pryshon na Bridget Blue.