
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jackie Chandiru amefunguka sababu za kuvunjika kwa kundi la Blue 3.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Chandiru amesema ugomvi wa kila mara kati yake na Cindy Sanyu ndio chanzo cha kundi hilo kuvunjika, jambo ambalo liliwafanya wasanii wa kundi hilo kuchukua maamuzi ya kufanya muziki kama wasanii wa kujitegemea.
Msanii huyo amesema iwapo wangetatua tofauti zao na Cindy mapema kundi la Blue 3 lingekuwa bado linaendelea harakati zake za kuwaburudisha mashabiki.
Hata hivyo amesema hana chuki dhidi ya msanii mwenzake Cindy Sanyu huku akisisitiza kuwa anaamini kuna kipindi watakuja kufanya kazi pamoja kama kundi.
Blue3 ni kundi la muziki kutoka uganda ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii watatu ambao Jackie Chandiru, Cindy Sanyu na Lilian Mbambazi.
Kundi hilo lilianza muziki mwaka wa 2004 baada ya kushinda tuzo ya Coca Cola Popstars Mwaka 2003 na lilivunjika rasmi mwaka wa 2009 baada ya kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki.