
Mwanamuziki Jackie Chandiru amefichua kuwa kuna uwezekano hatoshiriki katika uchaguzi ujao wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda (UMA) licha ya member wa zamani wa kundi la Blue3, Cindy Sanyu kugombea urais katika chama hicho.
Chandiru anasema anamuunga mkono Cindy lakini amehamua kukaa mbali na uchaguzi huo kutokana na manyanyaso aliyokumbana nayo alipokuwa chini ya kundi la Blue 3 ambalo lilikuwa linaongozwa na Cindy Sanyu.
βShuleni kuna mtu nilimuunga mkono lakini alipokua kiongozi wa darasa alianza kunionea. Sipendi kupiga kura kwa sababu watu hufanya kinyume na kile wanachoahaidi,β amesema kwa mafumbo kwenye moja ya mahojiano yake nchini Uganda.
Chandiru, hata hivyo, amesema Cindy ana sifa zote za kuwaongoza wanamuziki Β nchini Uganda kupitia chama hicho ila hatopiga kura.
Ujumbe huo umetafsiri na walimwengu kuwa msanii huyo bado ana machungu na Cindy ambaye walikuwa wanaunda kundi la Blue 3 ambalo lilifanya vizuri kwenye muziki nchini Uganda kati ya mwaka wa 2003 na 2008.