
Msanii wa Bongofleva Jay Melody amesema hatokuja kumuandikia msanii mwenzake wimbo wowote kwa kuwa kipindi cha nyuma hakufaidi na chochote kwenye shughuli ya uandishi ya nyimbo.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Jay Melody amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake zote kwenye suala la kujiandikia nyimbo zake mwenyewe kama njia ya kutanua wigo wa muziki wake huwafikia watu wengi duniani.
Lakini pia Hitmaker huyo wa βSugarβ amewataka mashabiki waache utimu kwenye muziki kwa kuwa inarudisha nyuma juhudi za wasanii kuupeleka muziki wa Bongofleva kimataifa.
Kwa sasa Jay Melody anafanya vizuri na ngoma yake mpya inaitwa βNakupandeβ.