Mchekeshaji anayekuja kwa kasi nchini Kenya, Jaymoh Decin, ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kutwaa tuzo ya heshima ya Comedian of the Year katika hafla ya utoaji wa tuzo za Pulse Awards 2025.
Jaymoh, ambaye amejizolea umaarufu kupitia video zake za kuchekesha kwenye mitandao ya kijamii, amesema ushindi huo ni matokeo ya bidii na kujituma katika kazi yake ya ucheshi. Alieleza kuwa ni neema kuona juhudi zake zikitambuliwa katika tasnia yenye ushindani mkubwa.
Kupitia ujumbe alioutoa baada ya kupokea tuzo hiyo, Jaymoh ameeleza kuwa anatoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa nguvu na uthabiti, akisema kuwa kazi yake ya ucheshi hatimaye imeanza kuzaa matunda na kufikia hadhira pana zaidi.
Ushindi wa Jaymoh Decin umeonekana kama ishara ya kizazi kipya cha wachekeshaji nchini Kenya kinachotumia ubunifu na mitandao ya kijamii kuinua tasnia ya burudani.