
Klabu ya Arsenal imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno, Joao Felix, kutoka Atletico Madrid mwezi Januari.
Hata hivyo watakutana na ushindani dhidi ya Paris St-Germain, Manchester United na Aston Villa ambazo pia zimeonyesha kuhitaji huduma ya nyota huyo.
Lakini pia Arsenal wataweza kumsajili winga wa Ukraine, Mykhaylo Mudryk, dirisha dogo la mwezi Januari kwa dau chini ya pauni milioni 86 ambalo Shakhtar Donetsk walilihitaji ili kumuachia mchezaji huyo.