
Msanii wa muziki wa Bongofleva K2ga ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Safari.
Safari EP ina jumla ya ngoma tatu za moto ambazo amezifanya bila kumshirikisha msanii yeyote. EP hiyo ina nyimbo kama Ni Wewe, Danga na Goma.
Safari ni EP ya kwanza kwa mtu mzima K2ga tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia digital platform tatu ambazo ni Youtube, Audiomack na BoomPlay.