
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga amefichua kuwa Rais Museveni ameshindwa kutimiza ahadi yake aliyotoa ya kumfadhili kusomea kozi ya uhandisi wa sauti nchini Marekani.
Akiwa kwenye moja ya interview, Hitmaker huyo wa “Kiboko” amesema kwamba Museveni alikubali kumfadhili kimasomo nje ya nchi walipokutana katika Ikulu ya rais mwaka wa 2020 ila kwa watu wake wa karibu wamekuwa wakimpa ahadi za uongo.
Kalifah Aganaga aliigura chama cha NUP na kutimukia NRM baada ya kushindwa kupata tiketi ya chama hicho ambayo ingemsaidia kuwania ubunge wa eneo la Rubaga Kusini.