Entertainment

KALIFAH AGANAGA ATILIA SHAKA MFUMO WA UCHAGUZI UTAKAOTUMIWA NA MUUNGANO WA WANAMUZIKI NCHINI UGANDA

KALIFAH AGANAGA ATILIA SHAKA MFUMO WA UCHAGUZI UTAKAOTUMIWA NA MUUNGANO WA WANAMUZIKI NCHINI UGANDA

Mwanamuziki wa dancehall kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga ametoa wito kwa muungano wa wasanii nchini humo kutofanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya kwa njia ya mtandao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kiboko” amesema wasanii wengi nchini humo hasa chipukizi wamefulia kiuchumi, hivyo hawana uwezo wa kununua vifurushi vya kupigia kura mtandaoni.

Utakumbuka Kalifah Aganaga ametia nia ya kugombea wadhfa wa unaibu rais katika muungano wa wasanii nchini uganda kwenye uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa muungano huo utakaofanywa hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *