Entertainment

KANYE WEST MBIONI KUZINDUA KAMPUNI INAYOJIHUSISHA NA VIFAA VYA KITEKNOLOJIA

KANYE WEST MBIONI KUZINDUA KAMPUNI INAYOJIHUSISHA NA VIFAA VYA KITEKNOLOJIA

Baada ya kukuvalisha viatu na mavazi ya aina yake kupitia chapa ya Yeezy, Kanye West yupo tayari kukuletea vifaa vya kiteknolojia.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Kanye ameripotiwa kulisajili kibiashara jina la ‘DONDA’ mnano Septemba 21 mwaka huu ambapo dhumuni ni kutengeneza vifaa kama Simu, (laptop), Tablets, Headphones na Bluetooth speakers.

Akiwa muumini mkubwa wa vifaa vya kampuni ya Apple, sasa Kanye West amedhamiria kuwa mshindani mkuu wa kampuni hiyo kubwa ya vifaa vya kiteknolojia duniani.

Kwenye DONDA, Kanye West amepanga pia kutengeneza Saa za mkononi pamoja na miwani za kisasa, vifaa vingine kama earbuds na wireless headset ambavyo vitakuwa sehemu ya bidhaa za DONDA.

DONDA ni jina la mama mzazi wa Kanye West ambaye alifariki dunia Novemba mwaka wa 2007 na amelitumia jina hilo kwenye album yake ya 10 ambayo ilitoka Agosti 29 mwaka huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *