Mfanyabiashara mwenye utata Khalif Kairo na mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii Phoina wamezua gumzo mitandaoni baada ya kunaswa kwenye video wakionyeshana mapenzi hadharani.
Katika video hiyo, ambayo imesambaa kwa kasi mitandaoni, wawili hao walionekana wakiwa kwenye moja ya kumbi za burudani jijini Nairobi, wakishindwa kujizuia na kuanza kupigana mabusu mbele ya umati wa watu.
Tukio hilo limechochea uvumi kwamba huenda wawili hao wako kwenye uhusiano wa kimapenzi, jambo ambalo hadi sasa halijathibitishwa rasmi na yeyote kati yao.
Mashabiki mitandaoni wamegawanyika kuhusu tukio hilo; wengine wakisifu uhusiano huo wakisema ni ishara ya mapenzi ya kweli, huku wengine wakidai huenda ni kiki ya kimtandao au kampeni ya kibiashara.