
Rapa Khaligraph Jones amekanusha madai yaliyoibuliwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa anatumia madawa kuuweka sawa mwili wake.
Hii ni baada ya rapa huyo kupost video Instagram akiwa gym huku akionekana anakunywa kinywaji ambacho kiliwaaminisha watu kuwa anatumia madawa.
Khaligraph amesema hatumii madawa kama jinsi watu wanavyodhani ila ilikuwa ni kinywaji laini cha kumuweka sawa wakati wa mazoezi.
Hitmaker huyo wa “Yego” Amesisitiza kwamba muonekana wa mwili wake umetokana na bidii yake ya kwenda gym kila mara.