
Kim Kardashian na Pete Davidson wamethibitisha rasmi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Mtandao wa Daily Mail imethibitisha hilo kufuatia wawili hao kuonekana pamoja wakiwa wameshikana mikono kimahaba Novemba 14 mwaka huu huko Palm Springs, California nchini Marekani.
Tetesi za Kim na Pete kutoka kimapenzi zilianza baada tu ya kipindi cha SNL mwezi uliopita ambapo Kim Kardashian alialikwa kama Host, baada ya hapo ilifuata mitoko ya kila siku wakiwa pamoja kwenye maeneo ya kula bata.