Entertainment

KING KAKA MBIONI KUACHIA EP YAKE MPYA MWISHONI MWA MWEZI NOVEMBA 2021

KING KAKA MBIONI KUACHIA EP YAKE MPYA MWISHONI MWA MWEZI NOVEMBA 2021

Rapa King Kaka ameweka wazi tarehe ambayo EP yake mpya iitwayo Happy Hour itaingia sokoni.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter King Kaka amesema Happy Hour EP itatoka rasmi Novemba 30 mwaka huu ingawa hajaweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye EP hiyo.

Hitmaker wa “Fight” amesema singo ya kwanza kutoka kwenye EP yake  ya Happy Hour ambayo wawashirikisha wasanii wa kundi la Wakadinali itaachia muda wowote kuanzia sasa.

Ikumbukwe Happy Hour EP kutoka kwa mtu mzima King Kaka ilipaswa kuachiwa rasmi  Oktoba mosi mwaka huu lakini ilishindikana kutokana na rapa huyo kujikita kwenye kuiweka sawa afya yake baada ya kuugua kwa kipindi cha miezi mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *