
Klabu mbili nchini Saudi Arabia zimeingia vitani kusaka saini ya mshambuliaji wa PSG, Leo Messi huku wakiweka dau nono mezani litakalomzidi, Cristiano Ronaldo wa Al Nassir.
Timu hizo mbili Al-Hilal (Riyadh) na Al Itihad (Jedah) zipo tayari kumlipa staa huyo wa Argentina euro milioni 350 kwa msimu huku wakiomba msaada kwa serikali kukamilisha ofa hiyo.
Licha ya timu hizo kuonesha nia lakini zipo kwenye adhabu ya FIFA kwa kufungiwa kutosajili hadi msimu ujao wa majira ya joto.
Inadaiwa kuwa Al-Hilal ilikuwa klabu ya kwanza kumuhitaji Cristiano Ronaldo lakini kutokana na adhabu hiyo ilipelekea mchezaji huyo kusalia Manchester United hadi mwezi Novemba.