Sports news

Kocha wa Algeria Atoa Onyo Kabla ya Mechi ya Mwisho CHAN

Kocha wa Algeria Atoa Onyo Kabla ya Mechi ya Mwisho CHAN

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Algeria, Magid Bougherra, amesema kuwa ni lazima kikosi chake kishinde mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Niger ili kuendeleza matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mtoano kwenye Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Mechi hiyo ya Kundi C itapigwa Jumatatu katika Uwanja wa Nyayo, Nairobi, ambapo Bougherra amesisitiza kuwa hatma ya Algeria iko mikononi mwao wenyewe. Kocha Bougherra amewataka wachezaji wake kucheza kwa bidii na nidhamu ili kuhakikisha wanafanikiwa kusonga mbele katika mashindano haya ya bara.

Kwa sasa, Uganda inaongoza kundi hilo kwa alama sita na itamenyana na Afrika Kusini kwenye mchuano wao wa mwisho. Algeria iko nafasi ya pili ikiwa na alama tano, sawa na Afrika Kusini walioko nafasi ya tatu, huku wakitofautiana kwa idadi ya mabao.

Timu za Niger na Guinea tayari zimeaga mashindano, na mechi zao za mwisho hazitakuwa na athari yoyote kwenye msimamo wa kundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *