
Kufuatia mjadala ambao anauendeleza mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi akipaza sauti juu ya wasanii wa Kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki, staa wa muziki wa dancehall Konshens ameamua kuuvunja ukimya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Konshens ameonekana kusikitisha na maneno makali ambayo Omondi amekuwa akitoa kwa wasanii wa kigeni kwa kusema kwamba mchekeshaji huyo ana machungu na ubaguzi kwa wasanii wa nje.
Hitmaker huyo wa “Pull Up” amesema sio kwamba wasanii nje wana njaa ya pesa ila ni upendo wa mashabiki wao ndio imechangia pakubwa wao kuja Kenya kufanya shows Kenya.
Konshens ambaye atarajiwa kufanya shoo kenya kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka ameahidi kuwa akitua kenya atatenga muda wake wakutane na Eric omondi ili asikilize lalama zake kwa kina.
Hata hivyo Eric Omondi amesisitiza kuwa sio kwamba anawapiga vita wasanii wa kigeni ila ana jaribu kuipigania tasnia ya muziki ili iweze kukubalika nchini.