Gossip

KRG THE DON AIREJESHA GARI AINA YA AUDI Q7 ALIYOMZAWADI MKE WAKE WA ZAMANI

KRG THE DON AIREJESHA GARI AINA YA AUDI Q7 ALIYOMZAWADI MKE WAKE WA ZAMANI

Msanii wa muziki wa dancehall nchini KRG the Don amechukua gari aina ya Audi Q7 ambayo alimzawadi aliyekuwa mke Linah Wanjiru kwenye kumbukizi yake ya kuzaliwa.

Kupitia instastory kwenye mtandao wa Instagram KRG the Don ameshare clip ikionyesha gari hilo na kusindikiza na caption inayosomeka “eti my private car Q7 ulinunua wapi? “, ujumbe ambao unaashiria kuwa vijembe kwa mke wake wa zamani Linah Wanjiru.

Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa akijinasibu kuwa ni millionea kipindi cha nyuma alinukuliwa kwenye moja ya interview akikanusha kuirudisha gari alilomzawadi mke wake huyo.

Ikumbukwe wawili hao walitenga mwezi Oktoba mwaka huu kwa madai ya udanganyifu kwenye ndoa yao ambapo KRG the Don alienda mbali zaidi na kufungua shauri la talaka mahakamani dhidi ya mke wake huyo.

Bosi huyo wa Cash group Entertainment alifunga ndoa na Linah wanjiru mwaka wa 2014 na wamejaliwa kupata watoto wawili kwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *