
Msanii Krg The Don ameibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake baada ya kudai kuwa huwa anawafuta matajiri na watu waliokaribu naye kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia Instastory yake amesema hana tabia ya kufuata kila mtu mtandaoni haswa kama hakufahamu na pia ukiwa umefulia kiuchumi.
Msanii huyo amejinasibu kuwa ikitokea amefanya hivyo itakulazimu umlipe Kshs. 250,000 ili aweze kukufikiria kama atakuweka kwenye orodha ya watu wa kiwango chake.
“Some random guy told me to follow him back simply coz I was next to him because ni fan wa KRG. I don’t follow random peeps kama I don’t know you personally or hauna kakitu, but ukifika bei ya $2K I will dearly follow back.”, Aliandika.