Mwanamuziki wa Kenya, KRG The Don, amewakashifu vikali viongozi na wananchi wanaochochea migawanyiko na chuki miongoni mwa Wakenya.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mitandaoni, KRG amesema kuwa ni aibu kwa viongozi na raia wanaofurahia au kuchangia mgawanyiko wa kitaifa badala ya kuhimiza umoja na mshikamano.
Msanii huyo ameeleza kuwa taifa haliwezi kusonga mbele endapo Wakenya wataendelea kugawanyika kwa misingi ya ukabila, dini au chama cha siasa. Amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuhubiri amani na maridhiano badala ya kugawanya wananchi kwa maneno na vitendo vya uchochezi.
Hata hivyo KRG The Don, amehimiza vijana kutumia nguvu zao katika kujenga amani na kuhamasisha umoja nchini Kenya. Ameongeza kuwa ni wajibu wa kila Mkenya kulinda utu na heshima ya taifa kwa kuepuka mijadala ya chuki na mizozo ya kisiasa inayoharibu umoja wa nchi.