
Nyota Kylian Mbappe wa Ufaransa amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kulikosa Kombe la Dunia 2022 huku likienda Argentina.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Mbappe ameandika; “Tutarudi tena,”
Kauli hiyo imechambuliwa kuwa matumaini ya Ufaransa ambao mara ya mwisho kutwaa kombe hilo ilikuwa 2018 wanayepeleka michuano ijayo 2026.
Mbappe ameibuka mfungaji bora akiwa na mabao 8 akifuatiwa na Lionel Messi wa Argentina mabao 7.