
Msanii wa muziki kutoka Uganda, Lady Mariam, amefunguka kuhusu maisha yake ya mapenzi, akieleza kuwa sasa yuko tayari kuhitimisha maisha ya upweke na kuingia kwenye ndoa.
Akipiga stori na runinga moja nchini kwao, hitmaker huyo wa Tindatine, amesema anatamani kuolewa, lakini si na mwanaume wa kawaida tu.
Anasema anatafuta mwanaume aliye na uwezo wa kifedha, akibainisha kuwa amepitia mahusiano mengi na wanaume wasiokuwa na uwezo wa kiuchumi, jambo ambalo limechochea uamuzi wake wa kuweka kipaumbele kwenye uthabiti wa kifedha.
Kwa maoni yake, amefikia hatua ya maisha ambapo hataki tena kurudia makosa ya zamani, na anataka mwenza anayeweza kumudu maisha vizuri.
Pia, Lady Mariam amesema kuwa angependa mwanaume huyo asiwe mkazi wa Uganda, akieleza kuwa mahusiano ya awali na wanaume wa nchini humo hayajamletea furaha wala maendeleo aliyokuwa akiyatarajia, kimapenzi na hata kimaisha.