
Staa wa muziki kutoka Uganda Leila Kayondo amejitenga na tuhuma za kutumia dawa za kulevya.
Katika mahojiano na Sanyuka TV amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani yanaenezwa na watu wasiomtakia mema maishani.
Mrembo huyo amewataka mashabiki zake kupuuza taarifa hizo huku akisema kuwa uvumi huo unasambaza na aliyekuwa mpenzi wake SK Mbuga ambaye amekuwa akiwakodisha watu mtandaoni ili wamharibia chapa yake ya muziki.
“I have seen allegations of people saying that I use drugs however, I am very sure that it is one person who is funding and spreadig such false propaganda.” ~ Leila Kayondo
Utakumbuka SK Mbuga na Leila Kayondo wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kuanzia mwaka wa 2011 hadi 2015 walipoachana kwa tuhuma za usaliti.