Entertainment

LIL WAYNE ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUTAKA KUMUUA MLINZI WAKE

LIL WAYNE ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUTAKA KUMUUA MLINZI WAKE

Idara ya polisi mjini California imeanzisha uchunguzi dhidi ya Lil Wayne kufuatia madai ya kumtishia Silaha bodyguard wake katika tukio ambalo limetokea nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa TMZ, moja ya walinzi wa rapa huyo amewaambia polisi kwamba Wayne aliingia kwenye majibizano na mlinzi wake akiwa nyumbani kwake mjini Hidden Hills, California. Sababu kubwa inayotajwa ni Lil Wayne kumtuhumu bodyguard huyo kwa kupiga picha na kuzivujisha kwenye media.

Aidha upande wa Lil Wayne umekanusha madai hayo kwa kusema hayana ukweli na Weezy hamiliki silaha.

TMZ inaendelea kuarifu kwamba Bodyguard huyo hana mpango wa kufungua mashtaka dhidi ya Lil Wayne lakini polisi wameamua kuingilia kati na kufanya uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *