
Rappa kutoka Marekani Ludacris anatarajiwa kutunukiwa Shahada ya Heshima kutoka Chuo Kikuu alichosoma cha Jimbo La Georgia.
Ludacris anatarajia kutunukiwa Shahada ya heshima ya Sayansi katika maswala ya muziki ‘Bachelor of Science degree in Music Management’.
Mkali huyo ambaye anatajwa miaka kadhaa nyuma aliacha kuhudhuria kwenye masomo chuoni hapo mara baada ya kusaini mkataba wake na Def Jam Records.
Hata hivyo, mwaka 2019 alianza kurudi chuoni hapo kusaidia wanafunzi kwenye maswala ya ujasiriamali katika tasnia ya muziki na filamu.