
Video vixen aliyegeukia muziki wa Bongofleva Lynn amemtaja ‘Simba’ kama ndiye Boyfriend wake kwa sasa.
Jina la simba limeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wameenda mbali na kuhoji huenda mrembo huyo ana mahusiano na Diamond Platnumz ambaye amekuwa akitumia jina hilo.
Katika hatua nyingine, Lyyn aliyetaja umri wake ni miaka 23, amesema hajawahi kuwa na mahusiano na msanii yeyote yule ingawa amekuwa akitongozwa sana na wasanii hao.
Mrembo huyo ambaye kwa wakati mmoja amewahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Tommy Flavour amefunguka hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram.