
Rapa kutoka Marekani Machine Gun Kelly haishiwi vituko, ameibuka na kutaka kumvisha Pete yenye miiba mchumba wake, Megan Fox.
Kwenye mahojiano na Jarida la Vogue, Machine Gun Kelly ambaye hivi karibuni alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo wa muda mrefu, amesema pete hiyo imetengenezwa kwa miiba na pindi tu mpenzi wake akijaribu kuivua basi atapata maumivu makali sana.
Kwa mujibu wa tovuti mbali mbali zinazotoa gharama ya vito vya thamani, pete hiyo inatajwa kuwa na thamani ya shilling million 38.6