Msanii wa arbantone, Mad G, amevunja ukimya wake kufuatia madai ya kutaka kuondolewa kwenye kundi la Wakudumu na VJ Patelo, ambaye amemtuhumu kuwa msaliti (snitch).
Akiwa kwenye moja ya show jijini Nairobi, Mad G amepuuzilia mbali vitisho hivyo akisisitiza kuwa hakuna mtu mwenye mamlaka ya kumfukuza kwenye kundi ambalo si mali ya mtu binafsi.
Mad G ameongeza kuwa madai ya kumtoa kwenye Wakudumu hayana msingi wowote na hayawezi kufanywa na mtu ambaye si mmiliki wa kundi hilo.
Kauli yake imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa muziki wa arbantone, huku wengi wakisubiri kuona mwelekeo wa mzozo huu wa kisanaa.