Entertainment

MAJIRANI ATANGAZA KUACHA MUZIKI KISA KUBEZWA NA WATU.

MAJIRANI ATANGAZA KUACHA MUZIKI KISA KUBEZWA NA WATU.

Msanii wa muziki nchini Majirani ametangaza kuacha muziki rasmi baada ya kukosa support kutoka kwa wakenya.

Kupitia waraka mrefu aliouchapisha kwenye mitandao yake ya kijamii majirani amesema ameahamua kuacha muziki kabisa kutokana na kubezwa na watu kipindi alikuwa anapitia magumu kwenye maisha yake.

Hitmaker huyo wa “Tukumbukeko” ameenda mbali zaidi na kutasanua kuwa kwa sasa amelazimika kutimukia nchini poland kwa ajili ya kutafuta riziki na kuendeleza masomo yake ambapo amedai amegeuki kazi ya ujenzi ambayo inamuingizia kipato kizuri.

Utakumbuka Majirani alifanya vizuri kwenye muziki wake akiwa chini ya lebo ya muziki ya Grandpa records lakini baada ya lebo hiyo kufungwa anadaiwa kuanza kutumia kila aina ya mihadarati kutokana na msongo wa mawazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *