 
									Timu ya Sofapaka FC imeonyesha ari kubwa ya kupambana baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mara Sugar katika mechi ya Ligi Kuu ya FKF iliyochezwa kwenye uwanja wa Dandora.
Mara Sugar ilianza kwa nguvu kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 57, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 68, na kuonekana kuwa njiani kuchukua alama tatu muhimu.
Hata hivyo, Sofapaka haikukata tamaa. Timu hiyo ilirudi mchezoni kwa bao la kwanza dakika ya 72, na kuendelea kushambulia kwa nguvu hadi kufanikiwa kusawazisha dakika ya 95, na hivyo kunyakua alama moja muhimu.
Kufuatia matokeo hayo, Mara Sugar sasa inashikilia nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 6, huku Sofapaka ikishika nafasi ya 13 ikiwa na alama 5.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa mechi kadhaa zenye ushindani mkali ambapo Tusker itachuana na Kariobangi Sharks, Ulinzi Stars itavaana na Bidco United, Shabana itaikaribisha AFC Leopards, huku Kakamega Homeboyz wakipambana na APS Bomet.
 
								 
             
             
                             
                             
                             
                             
                             
                             
                            