Entertainment

MEMBA WA SAUTI SOL POLYCARP OTIENO AZINDUA KITACHU CHAKE “WRITTEN IN THE STARS”

MEMBA WA SAUTI SOL POLYCARP OTIENO AZINDUA KITACHU CHAKE “WRITTEN IN THE STARS”

Member wa kundi la Sauti Sol Polycarp Otieno maarufu kama Fancy Fingers amezindua kitabu chake kipya kipya kiitwacho “WRITTEN IN THE STARS” ambacho kinaangazia chimbuko la mwafrika.

Polycarp Otieno  Ametumia Ukurasa Wake Wa Instagram Kuthibitisha Hilo ambapo amesema kwamba kitabu hicho kinaelezea historia ya mwafrika kwa njia ya fasihi aandishi.

Msanii huyo amesema amehamua kuja na kitabu hicho kwa sababu kwa miaka mingi kumekuwa na uhaba wa vitabu vya watoto vinavyoeleza historia ya mwafrika kwa kina na kupitia kitabu cha “WRITTEN IN THE STARS” watoto watajifunza mengi kuhusu utamaduni na chimbuko la mwafrika.

Kitabu chicho  kinapatikana kwenye majukwaa kadhaa ya kuuza vitabu mitandaoni ikiwemo App ya Sauti Sol iitwayo Hustle sasa.

Hata hivyo kundi la Sauti Sol limesema kwamba nakala za vitabu vya  “WRITTEN IN THE STARS”zinatarajiwa kupatikana kwenye nchini zote zilizoko Afrika Mashariki kuanzia Desemba 3 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *