Others

Morocco yafuzu hatua ya mtoani Kombe la Dunia

Morocco yafuzu hatua ya mtoani Kombe la Dunia

Wawakilishi wengine wa Afrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar, Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Canada kwenye mchezo wa mwisho wa kundi F.

Morocco imefuzu wakiwa vinara wa kundi hilo baada ya kufikisha alama 7 wakifuatiwa na Croatia na kuwaacha Ubelgiji na Canada wakiyapa mkono wa kwaheri mashindano hayo makubwa zaidi kwa mchezo wa kandanda ulimwenguni.

Morocco inakuwa timu ya pili kutoka Afrika kutinga hatua ya 16 bora baada ya Senegal kutangulia mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *