LifeStyle

Mrembo wa Kenya Aomba Msaada Baada ya Upasuaji wa Makalio Kuleta Madhara

Mrembo wa Kenya Aomba Msaada Baada ya Upasuaji wa Makalio Kuleta Madhara

Mrembo wa Kenya Lydia Wanjiru amewaacha wengi na masikitiko baada ya kuomba msaada kufuatia changamoto za kiafya anazopitia baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio.

Kupitia Insta Story zake, Lydia amechapisha picha akiwa katika mazingira ya hospitali, akifunguka kuwa makalio yake yameshindwa kupona kama ilivyotarajiwa.

Mrebo huyo, ameeleza kuwa kwa sasa anapitia kipindi kigumu kiafya, huku akisisitiza kuwa bado ana matumaini ya kupona licha ya maumivu na changamoto anazokumbana nazo.

Kauli yake imekuja siku chache baada ya kukiri hadharani kuwa amekuwa akipata taabu kwenda chooni pamoja na kushindwa kukaa chini kwa mud, hali inayodaiwa kusababishwa na matatizo yaliyotokana na upasuaji huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *