Gossip

Msanii Iyanii Afichua Kiasi cha Pesa Anachompa Mpenzi Wake Kila Mwezi

Msanii Iyanii Afichua Kiasi cha Pesa Anachompa Mpenzi Wake Kila Mwezi

Mwanamuziki Iyanii amefichua kuwa amekuwa akimpa mpenzi wake, anayejulikana kama Shes Kemunto, posho ya kila mwezi inayokadiriwa kuwa kati ya KSh150,000 hadi KSh200,000.

Akizungumza kwenye mahojiano, Iyani alisema hatua hiyo ni sehemu ya kumtunza na kumthamini mpenzi wake kwa mchango wake katika maisha yake ya kila siku.

Mkali huyo wa ngoma ya Donjo Maber, amesema kwamba anapenda kuhakikisha Kemunto anaishi kwa starehe bila kuwa na wasiwasi wa kifedha.

Hata hivyo, Iyanii amesisitiza kuwa mapenzi sio maneno bali ni vitendo vinavyoonyesha kujali. Kauli hiyo imezua maoni mseto miongoni mwa mashabiki mitandaoni, wengine wakimsifu kwa ukarimu wake huku wengine wakidai ni matumizi ya kupindukia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *