
Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya Zzero Sufuri ameweka wazi jina la album yake mpya atakayoiachia mapema mwaka 2023.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Hitmaker huyo wa Zimenishika amesema album yake mpya itaitwa “Fursa yako” na itazungumzia uhalisia wa maisha yake nje na ndani ya muziki.
Aidha amesema album hiyo ilipaswa kutoka mwezi Agosti mwaka huu lakini kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake alilazimika kuhairisha.
Ikumbukwe hii inaenda kuwa album ya kwanza kwa mtu mzima Zzero Sufuri tangu aanze safari yake ya muziki.