Entertainment

MSANII WA MUZIKI WA GENGETONE LIL MAINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

MSANII WA MUZIKI WA GENGETONE LIL MAINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Msanii wa muziki wa Gengetone nchini Lil Maina ametangaza kuacha muziki mara baada ya ngoma yake ya “Kishash” kufanya vizuri sokoni.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni msanii huyo ambaye amekuwa kwenye game ya muziki kwa miaka 3 amesema amechukua hatua hiyo baada ya kufanikisha moja kati ya ndoto yake ya kuachia hitsong,  hivyo ni wakati wake wa kupumzika na kuacha wasanii wengine waendelee.

Taarifa Lil Maina kustaafu muziki imewaacha mashabiki zake na mshangao kwani wengi wamekuwa na kiu ya kutaka kusilikiza nyimbo zake baada ya kuachia ngoma yake ya “Kishash” mwezi mmoja uliopita.

Baadhi ya mashabiki wa Lil Maina wanahisi huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa nchini ili aweze kuachia singo yake mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *