Msanii mtukutu kutoka nchini Uganda, Alien Skin, ameweka wazi msimamo wake baada ya kukumbana na wimbi la wakosoaji wanaomtaka aachane na muziki.
Akizungumza kupitia TikTok Live, bosi wa Fangone Forest amewajibu vikali wanaomkosoa, akisema hawezi kuacha muziki hadi pale atakapokuwa sawa kifedha.
Alien Skin amesema kuwa sababu pekee itakayomfanya aachane na muziki ni pesa. Amewataka wakosoaji wake wamwombee apate mafanikio badala ya kumkatisha tamaa. Kwa mujibu wake, muziki ndio njia yake kuu ya kujipatia kipato, hivyo haoni mantiki ya kuacha wakati bado hajafikia malengo yake.
Msanii huyo ameongeza kuwa amebadilika kitabia ikilinganisha na hapo awali, na anaamini anastahili kuungwa mkono badala ya kukosolewa kila mara.
Hata hivyo amesisitiza kuwa ataendelea kuachia nyimbo mpya bila kujali maoni ya watu, hadi atakapopata utulivu wa kifedha.