
Baada ya kuwepo kwa tetesi mtandaoni, sasa huenda ikawa rasmi kuwa mrembo Lori Harvey ana uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji kutoka nchini Uingereza Damson Idris na wanaonekana wenye furaha pamoja katika penzi lao.
Kupitia ukurasa wa instagram wa muigizaji Damson Idris amepost picha yao ya pamoja wakiwa kwenye pozi la kimahaba.
Ikumbukwe huyo si muigizaji wa kwanza kuwa na mahusiano na mrembo Lori kwani mahusiano yake yaliyopita alikuwa na muigizaji Michael B Jordan.
Mbali na wawili hao, mrembo Lori Harvey amewahi kutoka kimapenzi na rapa Future na Diddy na watu maarufu wengine.