Gossip

MWANAMUZIKI DR. BITONE AAPA KAMWE HATOREJEA UGANDA

MWANAMUZIKI DR. BITONE AAPA KAMWE HATOREJEA UGANDA

Msanii  anayesusua kimuziki nchini Uganda Dr. Bitone ameapa kutorejea nchini humo baada ya kusafiri nchini Uingereza wiki iliyopita kwa ajili ya onyesho la muziki.

Kupitia video aliyoiweka kwenye mitandao yake ya kijamii Dr. Bitone amesikika akisema “Kila kitu hapa ni kizuri. Ninawezaje kurudi Uganda? Samahani watu wangu wa Uganda,”

Ujumbe huo umetafsiriwa na wadau wa muziki nchini Uganda kuwa huenda msanii huyo ameangukia penzi la sugar mummy  ambaye atamsaidia kimaisha nchini Uingereza.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma Bitone alikuwa akichumbiana na mwanamama, Lydia Nabatusa, ambaye alikuwa anaishi nchini Sweden.

Lakini mwanamama huyo alikata mawasiliano naye kwa kile kinachotajwa kuwa msanii huyo alikuwa anapenda sana pesa zake badala kumuonyesha mapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *