
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jowy Landa amefunguka sababu za kutokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema anaogopa kuchumbiana na mwanaume akiwa anafanya muziki kwani atakuwa kizingiti kikubwa kwake kutunaua wigo kisanaa.
“Wanaume huwa wanatudhulumu sana ila mimi sina mpenzi kwa sasa. Hawa wanaume wanaweza kukuharibia shughuli zako za kimuziki”, Alisema kwenye mahojiano na runinga moja.
Jowy Landa amekuwa akihusushwa kutoka kimapenzi na meneja wake DJ Roja lakini amekuwa akipuzilia mbali madai hayo kwa kusema kuwa hayana ukweli wowote.