Others

Mwimbaji wa Bongofleva  Phina ajiunga rasmi na kampuni, Ziiki Media.

Mwimbaji wa Bongofleva  Phina ajiunga rasmi na kampuni, Ziiki Media.

Mwimbaji wa Bongofleva  ‘Phina’ amejiunga rasmi na kampuni kubwa ya usambazaji muziki barani Africa, Ziiki Media.

Kwenye uzinduzi rasmi uliofanyika jijini Johannesburg nchini South Afrika, Phina amesema anajisikia mwenye furaha na bahati kuwa miongoni mwa wasanii wa kike kutoka Tanzania kupata nafasi ya kipekee kufanya kazi na familia nzima ya Ziiki Media.

“Ushirikiano uliozaliwa hapa leo ni hatua kubwa sana kwangu kwani hizi ni aina za fursa ambazo nimekuwa nikizitamani kuzifanikisha kwa muda mrefu kwenye kaziyangu. Niko tayari kuiwakilisha Afrika kwenye jukwaa mbalimbali huku tukiendelea kuipeleka sanaa na muziki wa Tanzania na Afrikka mbele” alisema Phina.

Katika kumkaribisha Phina Ziiki Media, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Arun Nagar amesema kukutana na kipaji kama cha Phina ni nadra sana, uwezo wake wa sauti na kutawala jukwaa ni vitu vya kushangaza na kutamani kuona kwa wasanii wengi zaidi.

“Binafsi nina shauku ya kuona atafanya nini kwenye jukwa zingine. Sina shaka na uwezo wake wa kimuziki na nina imani ushirikiano wetu utadhibitisha mengi zaidi ambayo bado hatujayashuhudia kutoka kwake. Nina imani kubwa sana na safari hii na tunafurahi sana kumkaribisha kwenye familia ya Ziiki” alisema Arun Nagar.

Makubaliano hayo ya miaka minne yanalenga zaidi kuendeleza kipaji cha mwimbaji huyo, kukuza soko lake la muziki duniani kupitia usambazaji, pamoja na kukuza fursa mbalimbali za biashara ya Muziki.

Ziiki Media ni kampuni inayoongoza kwenye biashara ya usambazaji wa kazi za muziki barani Afrika na India kwa ushirikiano na kampuni kubwa ya muziki duniani Warner Music Group, huku ikitoa huduma kama usimamizi na usambazaji wa kazi za muziki, promosheni na usimamizi wa wasanii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *