
Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka kuhusu kupata tatizo la kuharibika kwa mimba yake (miscarriage), kwenye series iliyopewa jina la ‘My Pregnancy Journey’.
Nadia Mukami amesema ujauzito ule ulikuwa mchungu sana kwake kwani siku ya kwanza tu kujigundua kuwa ni mjamzito, alikuwa akiendesha gari kwenda kwenye baby shower ya rafiki yake.
Akiwa njiani, alishtuka na kupelekea kuigonga gari nyingine. Wakati yeye na mchumba wake Arrow Bwoy wakiendelea kulea ujauzito, Nadia anasema alimpoteza mtoto wake mnamo April 12, 2021.
Hata hivyo Mungu amekuwa mwema kwa mwimbaji huyo kwani alipata ujauzito mwingine na amejifungua salama Machi 24 mwaka huu.