
Mkali wa muziki nchini Naiboi anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na EP yake “Otero” ambayo tayari ina takriban mwezi mmoja tangu itoke rasmi.
EP ya “Otero” ambayo ndio EP ya kwanza kwa mtu mzima Naiboi tangu aanze muziki imefanikiwa kufikisha zaidi ya Streams laki 5 kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Naiboi amewashukuru mashabiki zake kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zinazidi kuonyesha mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi.
Oktoba 29 mwaka huu Naiboi aliwabariki mashabiki zake na EP yake ya kwanza iitwayo “Otero EP” yenye jumla ya mikwaju 9 ya moto, ikiwa na kolabo 6 pekee.