
Staa wa Bongofleva, Nandy ameweka wazi ratiba ya show zake katika kuufunga mwaka 2021 ambapo anatarajia kufanya show zaidi ya 15 ndani ya nje ya nchi.
Show za kimataifa atazifanya Nairobi, Kenya, Lagos, Nigeria, Dubai na Afrika Kusini.
Hatua hiyo ya Nandy inakuja baada ya hivi karibuni kutaanza ziara yake ya kimuziki nchini Marekani kuanza Machi hadi Aprili mwaka wa 2022 baada ya kuihairisha kwa mwaka mmoja.
Utakumbuka mapema mwaka jana mwimbaji huyo alitangaza ziara yake iliyoipa jina la Nandy USA Tour 2020 ambayo ingeanza Mei 22 hadi Juni 20, mwaka wa 2020, lakini akalazimika kuifutiliwa mbali kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona.